Isaiah 21:6-11

6 aHili ndilo Bwana analoniambia: “Nenda, weka mlinzi,
na atoe taarifa ya kile anachokiona.

7 bAnapoona magari ya vita
pamoja na kundi la farasi,
wapanda punda au wapanda ngamia,
na awe macho, awe macho kikamilifu.”

8 cNaye mlinzi alipaza sauti, “Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi,
kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa.

9 dTazama, yuaja mtu anayepanda gari la vita
pamoja na kundi la farasi.
Naye anajibu:
‘Babeli umeanguka, umeanguka!
Vinyago vyote vya miungu yake
vimelala chini vikiwa vimevunjwa!’ ”


10 eEe watu wangu, mliopondwa kwenye sakafu ya kupuria,
ninawaambia kile nilichokisikia
kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
kutoka kwa Mungu wa Israeli.

Unabii Dhidi Ya Edomu

11 fNeno kuhusu Duma: Mtu fulani ananiita kutoka Seiri,
“Mlinzi, usiku utaisha lini?
Mlinzi, usiku utaisha lini?”
Copyright information for SwhKC